#EFCBnews: Rais Dkt. John Pombe Magufuli amezindua Kituo cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi (Comprehensive Training Center - CTC) kilichopo Mapinga katika Wilaya ya Bagamayo Mkoani Pwani. Kituo hicho kimejengwa kwa msaada kutoka Jeshi la Ukombozi la Watu wa China kwa gharama ya Sh. Bilioni 67.87 na kitatumika kutoa mafunzo ya kijeshi ya kisasa yatakayowawezesha askari kukabiliana na vitisho vya kiusalama vya kisasa.
Post a Comment